Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Kiswahili Fasihi Simulizi Lessons and Notes

Jukumu la vichekesho na Sifa za michezo ya watoto

 (7m 6s)
5297 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jukumu la vichekesho
a) Kuburudisha hadhira kwa kuchekesha.
b) Kuelimisha kwa kuonyesha jambo la kijinga alilofanya mtu.
c) Njia ya kuwapatia watu riziki.
d) Hutumika katika hadithi kuifanya ivutie.
e) Kukejeli kitendo fulani kisichofaa.
Michezo ya Watoto/Chekechea
- Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.
Mifano ni kama:
a) Mchezo wa baba na mama
b) Kuruka kamba
c) Kujificha na kutafutana
Sifa za michezo ya watoto
a) Waigizaji ni watoto.
b) Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
c) Huandamana na nyimbo za watoto.
d) Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.


|