Vigezo vya Kuainishia Methali/Kuziweka Pamoja na kuzichambuaa) Mandhari/mazingira k.m. kilimo. -Ukipanda pantosha utavuna pankwisha. -Jembe halimtupi mkulima.b) Maudhui k.m. ulezi -Samaki mkunje angali mbichi. -Mcha mwana kulia hulia yeye c) fani/tamathali k.m. takriri-Haba na haba hujaza kibaba-Mtoto wa nyoka ni nyoka. d) Jukumu k.m. kuonye-Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.-Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.f) Maana k.m. sawa - Haraka haraka haina baraka.- Polepole ndio mwendo.