Hadithi za Kisalua/Kihistoria: mighani na sifa zakei) Mighani -Hadithi za mashujaa/majangina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wakamba.Sifa za Mighania) Huhusu mashujaa wa jamii fulani. b) Wahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maadui.c) Wahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika kivuli n.kd) Mhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maadui.e) Mhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu.f) Mighani huzungumzia matukio ya kihistoria. g) Kuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithini.