Umuhimu wa semi :a) Kuonya k.m methali, ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’b) Kukuza uwezo wa kufikiri k.m. vitendawili na chemsha bongo.c) Kutafsidi lugha au kupunguza ukali wa maneno k.m. nahau ‘jifungua’ badala ya ‘zaa’.d) Kuburudisha k.m. vitendawili, chemsha bongo na vitanza ndimi.e) Kuelimisha k.m. kutofanya mambo kwa pupa-mla kwa pupa hadiriki kula tamu.f) Kuongeza utamu katika lugha. g) Kuboresha matamshi k.m. vitanza ndimi.h) Kukuza lugha k.m misimu.