Maigizo ya kawaida:Sifa za Mwigizaji bora
Answer Text: Maigizo ya kawaidai) Michezo ya Kuigiza-Maigizo ambayo huwasilishwa na watendaji jukwaani mbele ya watu.Sifa za Mwigizaji boraa) Awe jasiri ili aweze kuigiza mbele ya watu/hadharani.b) Awe na ubunifu ili aweze kufanya uigizaji kuvutia.c) Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko.d) Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka.e) Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali.