Mambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano:a) Kueleza aina ya ngano kwa kuzingatia wahusika na maudhui -Ngano yaweza kuwa ya mazimwi na ya mashujaa kwa wakati mmoja. -Ngano yaweza kuwa hurafa, ya usuli na ya kiayari. b) Kutaja wahusikac) Kufafanua sifa za wahusika wakuu d) Maadili/mafunzo yanayojitokeza katika hadithie) Kubainisha sifa za ngano/hurafa/hekaya, n.k. zinazojitokeza katika hadithi. f) Kueleza umuhimu wa fomyula ya kuanzia/wimbo uliotumiwa katika hadithi.g) Kubainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika hadithi fulanih) Kuonyesha jinsi ngano inavyoshughulikia maudhui fulani.