Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Mhusika Boza na sifa zake katika tamthilia ya kigogo

 (4m 15s)
4555 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhusika Boza
Ni fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo, mumewe Asiya(mamapima)
1.Ni mwenye hasira.
Anamwambia Sudi kwa hasira kuwa embe lake linanuka fee.(uk1)
2.Ni kikaragosi.
Anatetea viongozi kuwa ni jukumu lao kusanya kodi,
kuwa huku ndilo kujenga nchi na kujitegemea.(uk3)
Anafurahia wimbo wa uzalendo unaosifia uongozi wa Majoka ilhali hali ni tofauti Sagamoyo kulingana na maudhui katika wimbo huo.
Anamuunga Majoka mkono ili afaidi.
3.Mwenye majisifu.
Anajisifu kuwa keki ya uhuru imeokwa na mke wake mwenyewe.
4.Ni msaliti.
Anawasaliti wanamapinduzi kwa kuunga mkono uongozi Mbaya wa Majoka mkono.


|