Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Uchambuzi wa onyesho la tatu,tendo la kwanza wa tamthilia ya kigogo

 (5m 41s)
3462 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Uchambuzi wa onyesho la tatu.
Tendo la kwanza
Ni ofisini mwa mzee Majoka, wana mazungumzo ya faragha na mshauri wake Kenga.
Njama yao ya kumtia Ashua ndani inatimia kisha wanamtarajia Sudi, achonge kinyago cha shujaa ndiposa Ashua aachiliwe.
Kenga anamwonyesha Majoka picha za
waandamanaji gazetini.Kuna habari kuwa Tunu aliongoza maandamano kisha kuwahutubia wanahabari kuwa:
-pesa za kusafisha soko zimefujwa,
-soko lilifungwa badala ya kusafishwa,
-haki za wauzaji zimekiukwa,
-hawatalegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.
Majoka anapanga kumwadhibu Tunu.
Maoni ya wengi gazetini ni kuwa,Tunu apigiwe kura za kuongoza Sagamoyo.Kenga anamshauri Majoka kutangaza kuwa maandamano hayo ni haramu kisha Polisi watumie nguvu, Majoka anapinga wazo hilo kwa kuwa;
maandamano yatatia doa sherehe za uhuru,
Tunu atazidi kupata umaarufu.
Wazo kuu:
Viongozi wanatumia mbinu tofauti kutawala;
-kupanga njama,
-kuadhibu waandamanaji,
-kutojali maslahi ya wanyonge.
Hata hivyo, wananchi wamezinduka na nia yao ni kubadili uongozi usiofaa.


|