Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Uchambuzi wa onyesho la sita,tendo la kwanza ya tamthilia ya kigogo

 (5m 39s)
2320 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Uchambuzi wa onyesho la sita.
Tendo la kwanza.
-Ni katika chumba cha wagonjwa, hali ya Majoka inaonekana kurejea.Anahukumiwa kuwa msaliti kwa wanasagamoyo na mashtaka mengine mengi.
Mayowe yanasikika na Majoka anadai kuwa hivyo ni vilio, wanalilia damu yakekisha Majoka
anazungumza na babu ndotoni.
-Majoka anawachukia marubani kwa kuwa waongo ilihali yeye pia ni rubani(kiongozi), hang`amui mambo kwa vile hajapambua ngozi yame ya zamani.
-Safari haijaanza au pengine chombo kinaenda kinyume badala ya mbele. Safari ya babu na Majoka inatofautiana, Majoka anashauriwa asalimu amri,
achague sauti ya moyo na babu yake.
Babu anamshauri Majoka afungue masikio, macho na moyo wake kwa kuwa maisha yana ncha mbili.
Kulingana na babu, kuna misimu ya fanaka na ya kiangazi, kadhia na kuishi kwa kutojali ni muhali.Mkwea ngazi huteremka hivyo mtu achague kutenda mema, kwa maana wema hauozi.Mtu akiishi kwa wema, atajiandikia tarijama njema huku ahera.
Wazo kuu. Maovu yana mwisho na kila aliye juu hatakaa juu milele.Wema ni muhimu katika maisha ya binadamu.


|