Ufaafu wa anwani ya tamthilia ya Kigogo
Answer Text: Ufaafu wa anwani ya tamthilia ya Kigogo-Kigogo ni mtu mwenye madaraka makubwa kiutawala.-Majoka anatumia madaraka yake kulaghai wananchi, anachukua vilivyo vyao.-Anatangaza kipindi cha mwezi mzima cha kusheherekea uhuru kutumia madaraka aliyonayo.-Majoka anafunga soko la Chapakazi ili sehemu hiyo ajenge hoteli ya kifahari kwa kutumia madaraka aliyonayo.-Anapandisha bei ya chakula katika kioskikwa vile ana madaraka.-Majoka anatumia mamlaka yake kumteka na kumtia ndani Ashua.Anamtendea ukatili, Ashua ana majeraha kutokana na kichapo.-Majoka anapanga kifo cha Jabali,mpinzani wake.Anampangia ajali na kuangamiza wapinzani wake pamoja na chama chake kwa kutumia mamlaka yake..-Majoka anapanga kutumia mamlaka yake kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu kifo cha Jabali.-Majoka anafuja pesa za kusafisha soko huku akijua hakuna wa kumhukumu kwa kuwa ndiye kiongozi.-Majoka anatumia mamlaka yake kudhibiti vyombo vya habari Sagamoyo,anasema sagamoyo kitabakia kituo kimoja tu cha habari;sauti ya mashujaa, vingine havina uhai.-Majoka kwa mamlaka yake anaamuru polisi kutawanya waandamanaji.-Majoka anampa mamapima kibali cha kuuza pombe haramu kwa kutumia mamlaka yake. Kwa mamlaka yake, Majoka anafadhili miradi isiyo muhimu, anafadhili mradi wa kuchonga vinyago kutoka nje.-Majoka anaamuru wafadhili wa wapinzani kuvunja kambi zao Sagamoyo.Anamfuta Kingi kazi kwa kutomtii apige watu risasi.