Mhusika Sudi na Sifa zake katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Mhusika Sudi na Sifa zake.Ni mumewe Ashua, fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo ambaye anashirikiana na Tunu kupinga maovu ya Majoka.1.Ni mzalendo.Kwake taarifa za Majoka hazimfai, za kutangaza mashujaa waliopigania uhuru Sagamoyo.Haoni maana ya uhuru huo hivyo kutomuunga mkono.2.Ni mwenye bidii.Anafanya kazi ya kuchonga vinyago kwa bidii.3.Ni mwenye msimamo thabiti.Licha ya kushawishiwa na kuhaidiwa mengi na Kenga ili achonge kinyago cha Ngao, anakataa na kushikilia msimamo wake.4.Ni jasiri.Anamwambia Kenga kwa ujasiri wamemulikwa mbali.(uk12).Haogopi kuchonga kinyago cha mwanamke.5.Amezinduka.Hali keki ya uhuru wanayoletewa na Kenga kwa madai kuwa ni makombo.Anaelewa kuwa viongozi wanawanyanyasa.6.Ni mwajibikaji.Sudi amewajibika,anajitahidi kwa udi na uvumba ili kumkidhi Ashua. Kila kitu anachokipata humletea Ashua.7.Ni mwenye mapenzi ya dhati .Sudi anampenda mkewe kwa dhati. Hufanya kila kitu ili kumkidhi.8.Ni mwaminifu.Sudi ni mwaminifu katika ndoa yake.Anampenda Ashua na anajelea kumpa talaka Ashua anapoiomba.9.Ni msomi.Sudi ana shahada, walisoma shule moja na Tunu.