Mbinu anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo
Answer Text: Mbinu anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo.Uvumi-.Watu wa Majoka wanaeneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.Ahadi za uongo-.Madai ya Majoka kuwa atatoa chakula kwa wasiojiweza si ya kweli. Kenga mshauri wa Majoka anawashawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao ili apate malipo mazuri na maisha yake kubadilika.Zawadi.- Kenga anawaletea Sudi, Boza na Kombe zawadi ya keki kuwafumba ili wamuunge mkono Majoka.Vitisho-.Wanasagamoyo wanatishwa kwa kurushiwawa vijikaratasi wahame. Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo.Matokeo yake ni watu kuhofia usalama wao.Mapendeleo-.Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika Majoka and Majoka academy akakataa, sasa angekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule za kifahari, viongozi hupendelea wengine kutumia njia sisizo halali.Jela-.Viongozi hufungia wanaowapinga jela.Ashua anatiwa ndani,kuna washukiwa wengi ndani.Polisi-.Majoka anatumia polisi kutawanya waandamanaji wanaodai haki zao. Viongozi hutumia nguvu.Majoka anadai wafadhili wa wapinzani lazima wavunje kambi zao Sagamoyo, kuwa Sagamoyo yajiweza.Ulaghai-.Majoka anapanga kuongoza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi. Kudhibiti vyombo vya dola.Majoka anapanga kufunga vituo vya runingasagamoyo ili abakie na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.