Wazo kuu na yanayojiri katika Onyesho la kwanza tendo la pili kwenye tamthilia ya kigogo
Answer Text: Tendo la pili.(Onyesho la kwanza)Katika karakana sokoni,Kenga anawatembelea Sudi, Boza na Kombe.Ametumwa na Majoka kuchukua vinyago vya mashujaa.Ni msimu wa mashujaa Sagamoyo, Sudi anachonga kinyago cha shujaa wa kike ambaye kwake ni kiongozi halisi wa Sagamoyo.Shujaa huyo hakufanya lolote, balianalifanya sasa katika jimbo la Sagamoyo.Miradhi ya kuchonga vinyago inafadhiliwa kutoka nje na wananchi wanatakiwa kulipa baada ya mwaka mmoja.Sudi anashawishiwa kuchonga kinyago cha Ngao ili maisha yake yabadilike na jina lake kushamiri;aidha apewe likizo ya mwezi mmoja ughaibuni.Sudianakataa kuchonga kinyago,Kenga anawapa keki lakini Sudi hali kwa kuwa ni makombo.Kombe anazinduka kutokana na kauli hii, anamuunga mkono Sudi.Kenga anaondoka kisha Tunu anawasili huku akihema na kusema kuwa mzee Kenga anapanga njama ya kuhutubia wahuni.Wote wanaondoka.Wazo kuu.Maskini wanatumikizwa, wanadhalalishwa, kuletewa makombo na kukumbukwa katika kipindi fulani tu ili kufaidi viongozi wao.Miradi isiyo muhimu inafadhiliwa na wananchi kupakia na jukumu la kulipa ufadhili huo kupitia kodi.Viongozi hushawishi wanyonge ili kuwatumikia.