Mhusika Ngurumo na sifa zake katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Mhusika Ngurumo na sifa zake.Ni kijana mpenda anasa, mfuasi wa Majoka.1.Ni mlevi.Ngurumo ni mlevi kupindukia,anajulikana Sagamoyo kutokana na ulevi wake.2.Ni msaliti.Anasaliti wanamapinduzi kwa madai kuwa Sagamoyo ni pazuri tangu soko kufungwa.Anasaliti katiba ya nchi yake kwa kunywa pombe haramu, kinyume na sheria.3.Ni mpenda anasa.Ngurumo anapenda anasa, kwake kulewa ni starehe.4.Mwenye taasubi ya kiume.Anamdharau Tunu kwa kuwa mwanamke,anadai kuwa yeye si kitu Sagamoyo.Anamwimbia wimbo wenye ujumbe kuwa aolewe ili asije akazeekea kwao5.Ni kikaragosi.Yeye ni mfuasi wa Majoka,anaunga uongozi wake mkono licha ya kuwa haufai.