Sifa za mhusika Majoka katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Sifa za mhusika Majoka.-Ni kiongozi wa jimbo la Sagamoyo.Ni katili.-Anaamuru Tunu auliwe,anavunjwa mfupa wa muundi.-Anamwambia kingi awapige watu risasi katika soko la Chapakazi.Ni mkware.-Anapanga njama ya kumpata Ashua, anamtakakimapenzi licha ya kuwa na mke na mtoto.Ashua anapofika ofisini mwake,anataka kumkumbatia na kumbusu.Mwenye hasira.Anakasirika Ashua anapokataa asimkumbatie na kusema kuwa hasira yake imeanza kufunganya virago.(uk 20)Mwenye majisifu.Majoka anataka sifa, anafurahi sana Ashuaanapomwita Ngao jina lake la ujana.-Anajisifu kuwa yeye pia anajua kuzaa na wala si kuzaa tu bali kuzaa na kulea.(uk22)Mwenye dharau.-Anawadharau watoto wa Ashua kwa kuwaita vichekechea.(uk22)-Anamdharau Sudi mumewe Ashua kwa kumwita zebe.Mpenda anasa.-Majoka anamwambia Ashua asilie bali aseme na ampendaye,astarehe kwenye kifua cha shujaa wake.(uk22)Mnafiki.-Anamwambia Ashua kuwa,"...haja zako ni haja zangu, shida zako ni shida zangu na kiu yako ni kiu yangu."-Nia yake ni kumteka Ashua kimapenzi, hana moyo wa kujali.Mpyaro.-Anawatusi wanasagamoyo kuwa wajinga katika soko la Chapakazi.-Anamwita Sudi mumewe Ashua Zebe.Mwenye kiburi.-Anajiita mwana wa shujaa kwamba ana akili ndipo kuwa mwana wa shujaa.Anasema kuwa aliitwa Ngao kwa kuwa na sifa.