Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Wazo kuu pamoja na yanayotokea katika onyesho la kwanza tendo la kwanza kwenye tamthilia ya kigogo

 (5m 34s)
7047 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Uchambuzi wa tamthilia “Kigogo” (Pauline Kea)
Onyesho la kwanza:Tendo la kwanza
Ni katika karakana ya soko la Chapakazi,Sudi, Boza na Kombe wanafanya kazi ya uchongaji.Sudi amefungulia redio huku wakiendelea na kazi yao.Ashua anawaletea chai ya mkandaa na mahamri na kuondoka.
Habari inatolewa kwa wananchi wa Sagamoyo kuwa wana kipindi cha
mwezi mzima kusheherekea uhuru wao, wawakumbuke majagina wao waliopigania uhuru na kuwanasua kutoka utumwani, wimbo wa kizalendo unachezwa mara kwa mara.
Sudi anatofautiana na mpango wa kusheherekea uhuru kwa mwezi mzima;kwake majagina wanaosheherekewa hawakufanya lolote katika historia ya Sagamoyo.
Kuna uchafuzi wa mazingira, viongozi hawajawajibika kusafisha soko wanadai kodi na kitu juu pia vitisho kwa wanasagamoyo.
Wazo kuu.
Kuna wale ambao wanaunga viongozi mkono kwa sababu wanafumbwa kwa mambo yasiyo ya kimsingi.Aidha kuna wale ambao
wamezinduka na kuhisi kuwa viongozi hawajawajibika. Sudi haoni umuhimu wa sherehe za uhuru kupewa maandalizi ya kifahali na kipindi cha mwezi mzima.


|