Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
OR
Processing. Please wait.
Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)
Matukio na wazo kuu katika tendo la pili onyesho la saba katika tamthilia ya kigogo
(4m 51s)
Download as pdf file
Answer Text:
Tendo la pili.(Onyesho la saba)
Ni katika lango la soko la Chapakazi, Majoka anawahutubia watu na kuwaita wajinga.Kenga anamnyang’anya kinasasauti.
Tunu anabebwa juu juu na watu, anawahutubia huku wakimpigia makofi.Amejitolea kutetea haki za wanasagamoyo ili;
-wapate maana halisi ya uhuru,
-watendewe haki,
-soko lifunguliwe na kujengwa upya,
-huduma muhimu ziletwe karibu kama vile; hospitali, barabara, maji, vyoo, nguvu za umeme, elimu, ajira kwa vijana na kadhalika.
Tunu anahimiza wanasagamoyo wachague viongozi wanaolinda haki za wanyonge na kuwajibika.
Majoka kwa hasira anaamuru watu wapigwe risasi,Kingi anapokataa kwa kuwa ni kinyume cha katiba kufyatua risasi anafutwa.Kenga anasalimu amri, anajiunga na umati.
Wazo kuu
Kila kilicho na mwanzo kina mwisho, uongozi wa Majoka unafikia nwisho.Juhudi za wanamapinduzi zimezaa matunda.Maana ya uhuru
sasa imepatikana na wananchi wanatarajia mengi mema.
|