Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Sifa za mhusika Tunu katika tamthilia ya kigogo

 (7m 9s)
6512 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sifa za mhusika Tunu
Ni mwanamke Sagamoyo ambaye anapinga maovu ya Majoka,rafikiye Sudi na mtoto wa Hashima.
1.Ni mwanamapinduzi.
Anaongoza maandamano Sagamoyo.
Anahutubia wanahabari kuhusu hali halisi Sagamoyo.
Anakiri kutolegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.
2.Ni msomi.
Ana shahada ya sheria kutoka chuo kikuu.
3.Ni mtetezi wa haki .
Anapanga kuleta wachunguzi kutoka nje ili kuchunguza kuhusu kifo cha Jabali .
Anamwambia Majoka wazi kuwa kila mtu Sagamoyo ana haki ya kuishi.
4.Mwenye msimamo dhabiti.
Anakataa wazo la Majoka kumwoza kwa Ngao Junior.
Licha ya kuumizwa mguu, halegezi kamba kuwapigania wanasagamoyo.
5.Ni jasiri.
Haogopi yeyote, anataka kukutana na viongozi katili ili awakashifu.
Anamwambia Majoka wazi kuwa hawezi kuolewa na mhuni,kwamba wanakula watu kwa jina la ugatuzi.(uk42)
6.Ni mzalendo.
Tunu anapigania haki za Wanasagamoyo, anamwambia Majoka kuwa wanasagamoyo wana haki ya
kuishi na kuwa ugatuzi si unyakuzi.
7.Mdadisi.
Anamdadisi mamake ili ajue maana ya ndoto ya Mzee Marara kumfukuza ili amnyang’anye mkufu wake wa dhahabu.
Anapanga kuchunguza ajali iliyosababisha kifo cha Tunu.
8.Mwajibikaji.
Tunu amawajibika, anaelewa athari ya pombe,na kukataa pombe anayopewa kwa mamapima.


|