Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Uchambuzi wa onyesho la tano,tendo la kwanza wa tamthilia ya kigogo

 (5m 23s)
2326 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Uchambuzi wa onyesho la tano.
Tendo la kwanza.
-Ni katika hoteli ya Majoka and Majoka modern resort, Husda anafika kutoka kuogelea.Kenga naye anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga,Tunu hakuvunjwa mguu.Chopi anapangiwa kwenda safari kwa kutotekeleza njama hiyo.
Sokoni, taka zote zimeondolewa, vibanda vimeng`olewa, vifaa vya ujenzi vimewasili kutoka bandarini na kuna ulinzi mkali.
-Chopi anafika na habari mbaya kuwa Ngurumo amenyongwa na chatu akitoka Mangweni.Majoka anaagiza Ngurumo azikwe kabla ya jua kutua.
Ushauri wa Majoka ni kuwa chatu mmoja atolewe kafara, na baada ya watu kuandanana waachwe katika hali ya taharuki.
Wazo kuu.
-Viongozi hupanga njama za kuwaangamiza wapinzani wao.
-Viongozi wanaishi maisha ya kifahari huku maskini wakihangaika.
-Viongozi hawajali hata vifo vya wananchi vikitokea.


|