Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
OR
Processing. Please wait.
Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)
Maudhui makuu katika tamthilia ya Kigogo -Pauline Kea
(21m 24s)
Download as pdf file
Answer Text:
Maudhui makuu katika tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)
1) Uongozi mbaya.
-Viongozi huangaisha wanyonge,Ashua anasema, "...na kuhangaishwa na wenye nguvu ndio hewa tunayopumua huko." (uk 2)
-Wachochole hutumikizwa na viongozi, Kombe, Boza na Sudi wanafanya kazi ya kuchonga vinyago vya mashujaa kwa ajili ya sherehe za uhuru.
Viongozi hawajawajibika, kazi yao ni kukusanya tu kodi.Ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa soko ni safi lakini hawajawajibika kulisafisha. Licha ya wananchi kutoa kodi,soko ni chafu.(uk 2)
-Viongozi kutangaza kipindi kirefu cha kusheherekea uhuru ni ishara ya uongozi mbaya.Mashujaa
wanaenziwa kwa kipindi kirefu ilhali mambo ya kimsingi hayajazingatiwa.Wanasagamoyo wana matakwa mengi kuliko kipindi kirefu cha kusherehekea uhuru.
2) Uzalendo wa wananchi
-Wananchi wa Sagamoyo ni wazalendo, wanalipa kodi ili kuleta maendeleo licha ya kulaghaiwa. Katika enzi za ukoloni, mashujaa walijitolea mhanga wakahatarisha maisha yao na hata kufa ili wavune matunda baada ya uhuru. (uk 4) Wimbo unaoimbwa katika rununu ni wa kizalendo kuonyesha kuwa wanasagamoyo wanalipenda jimbo lao, sagamoyo.(uk 5) Sudi anaelewa kuwa uongozi wa Majoka haufai.Anawaeleza Boza na
-Kombe umuhimu wa kuandika historia ya Sagamoyo upya.Kinyago anachokichonga Sudi ni cha shujaa halisi wa Sagamoyo,anaelewa kuwa Tunu ndiye anapaswa kuwa kiongozi halisi.
-Tuni ni mzalendo katika taifa lake. Anasema kuwa jukumu lake ni kulinda uhai, haki na uhuru.Amajitolea kwa vyovyote vile kutetea haki Sagamoyo.Wamekula kiapo kutetea haki Sagamoyo hata kama ni kwa pumzi zao za mwisho baada ya mafanikio. (uk18)
3) Nafasi ya mwanamke katika jamii.
Sudi anapochonga kinyago cha shujaa mwanamke,Kenga anamwambia Sagamoyo haijawahi kuwa na shujaa mwanamke.Katika historia ya Sagamoyo wanawake wametengwa katika uongozi.(uk 10).
Kenga anasema kinyago hicho hakitanunuliwa na afadhali achonge kinyago cha Ngao.
Wanawake wamesawiriwa kuwa hawara,Sudi anapokataa kuchonga jinyago,Kenga anamwambia kuwa amelishwa kiapo na hawara wake.(uk12)
Wanawake hutumiwa kama pambo katika jamii ya
Sagamoyo.Majoka anamwambia Ashua kuwa,urembo wake hauna mfanowe.
"...nikufanishe na nini? urembo wako hauna mfanowe Ashua"(uk 20)
Majoka anamshauri Ashua atumie urembo wake kwa kuwa ni wa muda.(uk 25)
Husda anakiri kuwa mwanamke ni pambo mbele ya mwanamume.(uk67)
Wanawame wamesawiriwa kuwa wenye maringo.Majoka anadai kuwa Ashua alikataa kazi ya ualimu kwa sababu ya maringo.(uk25)
4) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
-Majoka anatunia polisi kuwatawanya waandamanaji na kuwaumiza wapinzani wake,Tunu anaumizwa mguu.
Runinga ya mzalendo haina maisha Sagamoyo kwa sababu ya kupeperusha habari za maandamano. Majoka anaamua kufunga vituo vya habari na kibakie tu kituo kimoja.
-Kenga anamshauri Majoka waichukulie hatua runinga ya mzalendo kwa kuwa haimpendi yeye. Majoka anatumia vyombo vya habari kuimba nyimbo
za kizalendo ili kumsifu yeye.
-Vyombo vya habari hueneza propaganda,kuna habari katika vyombo vya habari kuwa Tunu hawezi kupigania haki za Wanasagamoyo kwa kuwa amelemazwa mguu.
5) Asasi ya ndoa
a) Ndoa kati ya Ashua na Sudi.
Ni ndoa yenye mapenzi yanayoegemea upande mmoja.Sudi anampenda Ashua kwa dhati,anajitahidi kwa udi na uvumba ili kumkidhi Ashua.Kila kitu anachokipata humletea.
Sudi ni mwaminifu katika ndoa yake,hajamwenda Ashua kinyume hata Ashua anapotiwa ndani na Majoka. Aidha, ndoa hii imejengwa katika misingi ya kutoaminiana.Ashua anamshuku mumewe kuwa ana mipango ya kimapenzi na Tunu.
b) Ndoa kati ya Majoka na Husda.
-Ni ndoa ambayo imejaa lawama,Majoka anamlaumu Husda kuwa hampendi bali aliolewa na mali yake.( uk 75)
Hakuna mapenzi ya dhati katika ndoa hii.Majoka hampendi Husda. Alimoa ili kutimiza wajibu wake katika jamii na kama kiongozi,alipaswa kuoa.Alilia usiku huo baada ya kumwoa Husda lakini moyo na nafsi yake viko kwa Ashua.(uk75)
6) Ulevi na athari zake
-Mangweni kwa mamapima shughuli za ulevi zimeshika kani.
-Ngurumo ni mlevi kupindukia, anajulikana
Sagamoyo kwa uraibu wake wa vileo.Anakunywa pombe zaidi ili kusherehekea sherehe za uhuru.
-Vijana ni walevi kwa mamapima hadi wanasimama kwa taabu.
Ulevi umepotosha baadhi ya vijana,Ngurumo alisoma darasa moja na Tunu lakini ni mlevi kupindukia, hajitambui.
Kwa mamapima kila mtu hupewa vileo kwa raha zake.
-Ulevi umemfumba Ngurumo hadi haoni athari za soko kufungwa,yeye anadai kuwa yuko sawa na hataki soko lifunguliwe.(uk60)
|