Matukio na wazo kuu katika Onyesho la tatu, tendo la tatu ndani ya tamthilia ya kigogo
Answer Text: Tendo la tatu.(Onyesho la tatu)Ni ofisini mwa mzee Majoka,Tunu na Sudi wanaingia.Majoka anataka kusema na kila mmoja lakini wanakataa kwa kuwa na nia moja.Sudi anaarifiwa kuwa Ashua mkewe yuko ndani kwa kuleta fujo katika ofisi ya kiserikali.Majoka anamshawishi Tunu kuwa amampangia jambo la kifahari, kumwoza NgaoJunior atakaporejea kutoka ng`ambo.Tunu hakubaliani ma kauli hii, anamkabili Majoka na kumwambia ukweli kuwa wao ni wahuni na wauaji.Tunu anatishiwa kutiwa ndani.Tunu anafichua ukweli, Majoka walipie kila tone la damu waliyomwaga Sagamoyo.Wao kuu.Viongozi hushawishi wapinzani kwa ahadi ili wawaunge mkono,hata hivyo wanamapinduzi wanashikilia msimamo wao.