Matakwa ya wanasagamoyo katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Matakwa ya wanasagamoyo.-Soko ambalo ni tegemeo lao linafungwa.Waataka soko lao lifunguliwe na kujengwa upya pia lisafishwe.-Hawana usalama,askari wanatumiwa kuwatawanya na kuwatishia.Wanaishi kwa hofu.-Hawana uhuru wa kutangamano kwani viongozi wao wanahofia maandamano.-Haki zao zimekiukwa.Mauaji yanapangwa kwa njama za kuwaangamiza.-Wanataka kujengewa hospitali, barabara na vyoo.Waletewe nguvu za umeme.-Wanataka wapate elimu Sagamoyo na ajira kwa vijana.-Wanasagamoyo wana njaa-Walimu na wauguzi Sagamoyo wana mishahara duni.-Kuna vilio Sagamoyo,mauaji yanapangwa.Wanasagamoyo wanataka mauaji haya yakome na haki kutendwa.-Wanasagamoyo wananyanyaswa na viongozi, bei ya chakula inapandishwa ilihali wengi wa wananchi ni maskini.-Mazingira Sagamoyo ni chafu hadi kuhatarisha maisha yao.Wanataka soko kusafishwa.