Uchambuzi wa onyesho la pili,tendo la kwanza katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Uchambuzi wa onyesho la pili.Tendo la kwanza.-Ni ofisini mwa Mzee Majoka, anaongea kwa simu Chopi anapoingia.Ashua anafika kumwona Majoka,anataka kumkumbatia lakini Ashua anakataa.Majoka anakasirika Ashua anapomwita mzee na kufurahi anapomwita Ngao, jina lake la ujana.Ashua amefika kuomba msaada lakini Majoka anamtaka kimapenzi.Anajaribu kumbusu lakiniAshua anakwepa.Majoka anamshawishi, anajisifu na kujilinganisha na Lyonga wa uswahilini na Samsoni Myahudi.-Majoka anasema kuwa soko limefungwa kwa sababu ya uchafu, anatenga eneo hilo ili kujenga hoteli yakifahari.Wanasagamoyo wanalitegemea soko hilo kula, kuvaa na kuendesha maisha yao.-Ashua anakataa kazi ya ualimu anayopewa Majoka and Mahoka academy, angekuwa mwalimu mkuu katika shule mojawapo ya kifahari.Wazo kuu.-Viongozi hunyanyasa wachochole ili kujifaidi,Majoka anafunga soko na kunyakua eneo hilo kujijengea hoteli ya kifahari.Anataka kutumia mali na mamlaka yake kumteka Ashua kimapenzi.