Uchambuzi wa onyesho la saba,tendo la kwanza ya tamthilia ya kigogo
Answer Text: Uchambuzi wa onyesho la sabaTendo la kwanza.-Ni katika uwanja wa ikulu ya Majoka palipoandaliwa sherehe.Ni saa nne na watu kumi tu ndio wamefika, wengine wako sokoni.-Sauti inasikika kwa mbali watu wakimsifu Tunu.Majoka anaelekea ilipo sauti,Kenga na umati wanawafuata.Wazo kuu.-Wananchi wana nguvu zaidi kuliko viongozi .Wananchi wana mchango mkubwa kujikomboa kutokana na shida wanazozipitia zinazoletwa na uongozi mbaya.-Ili kujenga jamii mpya, wanachi hawana budi kuzinduka na kuleta mapinduzi.