Wazo kuu na matukio katika Onyesho la tano, tendo la pili ya tamthilia ya kigogo
Answer Text: Tendo la pili.(Onyesho la tano)-Ni ndani ya ambulensi,Majoka hataki kufungua macho kuliona ziwa la damu.Majoka anasema yuaelekea jongomeo, kuwa amefungwa minyororo.Anataka safari isitishwe kwa kuwa haina stara.-Majoka anamfananisha Husda kama mke anayeishi ndani ya ngozi ya kondoo(kuwa Husda ni mnafiki).Husda anapenda mali ya Majoka na alilazimishwa kumwoa lakini moyo wake unampenda Ashua.-Daktari anamjuza Husda kuhusu kifo cha Ngao Junior,anazirai.Wazo kuu.-Asasi ya ndoa imesawiriwa kuwa na changamoto;Husda hakumpenda Majoka ila aliolewa naye kwa sababu ya pesa. Ili kuokoa asasi ya ndoa, wanaume wanapaswa kujidadisi, wawe na heshima na waseme na wake zao.Wake nao wajirudi ili ndoa zidumu.