Sifa za Ashua katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Sifa za AshuaNi mkewe Sudi,mamake Pendo na Pili1.Ni mwenye msimamo thabiti.Licha ya kushawishiwa kimapenzi na Majoka, hakubaliani na kauli yake.Anashikilia msimamo wake kuwa ana mume na hataki kuvunja ndoa yake,anakataa huba kutoka kwa Majoka.2.Ni jasiri.Anamkabili Majoka kwa kupasa sauti ofisini mwake,haogopi.Anamwambia kwa ujasiri kuwa anefika kwake kuomba msaada.3.Ni mnyenyekevu.Ananyenyekea mbele ya Majoka ofisini mwake na kumwomba msamaha,anamwomba Majoka amkanye Husda asimtusi.4.Ni mwenye heshima.Anakiri kuwa anamheshimu Majoka.5.Ni mwaminifu.Ashua ni mwaminifu katika ndoa yake. Anakataa kufanya mapenzi na Majoka kwa kuhofia talaka yake.Anathamini ndoia yake, anakataa pendekezo la Majoka kwa madai kuwa yeye ni mke wa mtu.6. msomi.Ashua amesoma na ana shahada ya ualimu.7.Amezinduka.Anadai kuwa kampuni ya Majoka ni ya wahuni.Anaelewa kuwa wanasagamoyo wamenyanyaswa hivyo kujiunga na wanamapinduzi kupigania haki.8.Ni mkali.Ashua anamkabili Husda kwa ukali ofisini mwa Majoka.