Mhusika Kenga na sifa zake katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Mhusika Kenga na sifa zake.Ni mshauri mkuu wa Majoka.1.Ni mshauri mbaya.Anamshauri Majoka visivyo.Anamwambia atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha aamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.2.Ni kikaragosi/KibarakaAnamuunga Majoka mkono hata kwa mambo yasiyofaa nia yake ikiwa ni kujinufaisha kutokana na uongozi wake.3.Ni fisadi.Yeye na Majoka wanadai kitu kidogo kutoka kwa wanasagamoyo. Baada ya soko kufungwa,Majoka anamwambia kuwa kipandechake cha ardhi kipo.Anakipata kwa njia isiyo halali.4.Ni mwoga.Kenga anahofia maandamano yanayoendelea na kumshauri Majoka asiyapuuze5.Ni mwenye matumaini.Hafi moyo, anasema atarudi tena na tena ili kusema na Sudi ili achonge kinyago.