Umuhimu wa Tunu katika tamthilia ya kigogo
Answer Text: Umuhimu wa Tunu:-Tunu ametumika kuonyesha kuwa kuna wazalendo katika jamii ambao wamejitolea kupinga uongozi mbaya ili kuleta haki na usawa katika jamii.-Mwandishi amemtumia mhusika Tunu kuonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mtoto wa kike, bado ana nafasi muhimu katika ujenzi wa jamii mpya, wanawake ni muhimu katika uongozi ili kuleta maendeleo.Aidha, anawakilisha umuhimu wa kuungana kwa vijana ili kuleta mabadiliko katika mataifa yao.