Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Mbinu za sanaa katika riwaya ya chozi la heri

 (13m 28s)
14497 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
MBINU ZA SANAA KATIKA RIWAYA YA CHOZI LA HERI.
(a) KINAYA
- Hii ni mbinu inayofanya matukio katika kazi ya Sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.
- Katika ukurasa wa 5; "Naona umeanza kuitia akili yangu kwenye
mtihani mgumu. Unanichanganya hasa! Kwanza sijui wapi kapata mtoto wa miaka hamsini". Ni kinaya kuwa mtoto ana miaka hamsini, kinyume na matarajio ya kawaida ya kuwa mtoto ni yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na minane.
- Katika ukurasa wa 62; Mwangeka aliajiriwa na kupanda ngazi moja baada ya nyingine hadi alipoenda kudumisha amani kwingine, na mkewe kufa kutokana na ukosefu wa usalama nchini mwao huu ukawa mwisho wa ndoa yao ya miaka mitatu.
(b) SADFA.
- Sadfa ni mgongano wa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vimepangwa, japo havikuwa vimepangwa.
- Katika ukurasa wa 175; "Tesi!sadfa gani hii? Unafanya nini hapa? Ulikuja lini jijini humu? Yu
wapi wifi Nema? Niliskia mtoto wenu amehitimu chuoni!
- Katika ukurasa wa 175; "Nakumbuka sana. Na kweli hii ni sadfa kwa sababu pia ni siku ya kuzaliwa kwa binti yangu Umulkheri ".
(c) NYIMB0.
- Ni maneno na sauti zilizopangwa na huandamana na muziki unaotokana na ala za kimuziki kama vile ngoma. Sauti hizi za muziki pia huwa zimepangwa ili kuandamana na maneno vizuri na kwa urari.
- Katika ukurasa wa 20; "Wote walikuwa wakighani mkarara huu: Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi wetu tawala Waha.
- Katika ukurasa wa 49; "Mama mtu angemshika mabegani na kumwimbia mkarara mmoja wa wimbo pendwa wa kidini:
Salama, salama
Rohoni, rohoni
Ni salama, rohoni mwangu"
(d) MATUMIZI YA BARUA
- Lunga anapokea barua rasmi ya kumfuta kazi. Ni fupi lakini yenye ukali na kukatisha tamaa (Uk 72;). Barua yenyewe iliandikwa na bwana Kalima ambaye
alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya kitaifa ya uhifadhi wa nafaka.
- Naomi (uk 81) Mkewe Naomi anamwambia kuwa ameondoka. Ameenda kutamba na ulimwengu, na huenda akaambulia cha kumsaidia mumewe kuikimu familia yao.
- Mwanaheri alipoisoma barua ile, alihisi kuwa imejaa ujumbe wa mauti (UK.95). Barua hii inaandikwa tarehe mbili mwezi wa sita mwaka wa elfu mbili na tisa. Inaandikwa kwa mpenzi wake Mwanaheri. Anasema kuwa, Mwanaheri atakapoisoma
barua ile, labda yeye hatakuwa hapo au pia katika ulimwengu huu.
(e) TAHARUKI
- Hii ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya kwa kufanya hadhira au wasomi wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka
kuendelea kusoma. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kulazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali.
- Katika ukurasa wa 19; "Mijadala hii ilizua na kukuza migogoro isiyomithilika. HaIi ya taharuki ilitamalaki,
vyombo vya dola vikatumwa kudumisha usalama.
- Katika ukurasa wa 152; "Usinitazame kana kwamba unataka nikwambie yaliyotokea baadaye, 'nilijisemea kana kwamba ninajibu mtazamo wa ndio
kuniambia kwani nilijipata hapa penu.
(f) NJOZ1 AU NDOTO.
- Mwandishi hutumia njozi au ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.
- Katika ukurasa wa 2; "Anakumbuka
akimwambia mkewe Terry, "Milio hii ni kama mbiu ya mgambo, huenda kukawa na jambo. "Terry kwa ucheshi wake wa kawaida hakunyamaza”. "Ridhaa akamwambia, "wewe endelea kupiga hulu tu, lakini utakuja kuniambia!"
- Ridhaa alikuwa na ndoto ya kuwa kuna jambo mbaya au lisilo la kupendeza ambalo lingeweza kutendeka, na kwa kweli, njozi lake likawa ni la ukweli wakati lilipotimia.


|