Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Sura ya tatu katika chozi la heri na yanoyojiri

 (10m 13s)
12725 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya tatu:
-Baada ya kuishi katika msitu wa Mamba kwa miezi sita, Ridhaa, Kaizari na familia yake walibahatika kurudi nyumbani kufuatia mradi wa Operesheni Rudi Kanaani.
- Asubuhi hii Ridhaa ameketi katika chumba cha mapokezi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Rubia. Ana hamu kuu ya kumwona Mwangeka akiwa mzima. Ridhaa anakumbuka kuwa siku ya kuhawilishwa kutoka Msitu wa Mamba hakuwa na matumaini ya maisha
bora kwani hakuwa na mwenzi wala mtoto wa kuendea.
-Wengine kama Selume walikuwa wakilia kwa kuwa hawakujua waende wapi kwani mme
wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao na Babake alimkatalia katakata. Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena
ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea.
-Ndipo Ridhaa akamwahidi warudipo nyumbani, angemtambulisha Selume kwa mkuu wa Idara ya Afya ya Jamii katika Hospitali Kuu ya Tumaini. Leo hii, Ridhaa anapowaza haya, Selume amekwisha kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali ndogo iliyojengwa karibu na kambi ya WWHN. Ridhaa anakumbuka mambo mengi kama vile kadhia iliyompoka familia yake ndiyo ilimkutanisha na watu kama Selume arnbao angewaita ndugu na kumfanya kusahau msiba wa kUipoteza akraba yake. Kaizari- amepona donda lilitokana na kuwaona binti zake wakibakwa. Ridhaa anamwona Kaizari ni afadhali kwani heri nusu Shari kuliko Shari kamili.
-Asubuhi hii, Ridhaa akiendelea kumngojea Mwangeka hakuweza kusahau jinsi alivyohisi aliporudi tena kwenye ganjo lake siku ile. Anakumbuka kuwa alipozinduka( kutoka kuzirai), alijipata katikati mwa kiunzi cha sebule lililokuwa kasri lake.
-Eneo hili ndipo wanawe Tila na Mwangeka walipokuwa wadogo walipenda kumkimbilia kila mara alipotoka kwenye shughuli zake za kikazi. Hapo ndipo kijukuu chake kilipozoea kutembea tata na
kumwita "bubu" naye alipenda kukirekebisha na kukiambia "sema babuu". Hayo yote hayapo sasa, hata zile pambaja za mkewe Terry na utani wake
hamna. Hatimaye ndege kwa jina PANAMA 79 iliyotarajiwa kufika saa tatu unusu sasa ndio inalikanyaga sakafu. Abiria
waliposhuka, Ridhaa na Mwangeka walitazamana kimya.
Ridhaa alihisi kana kwamba anauona mzuka wa Mwangeka, hakuamini kuwa angerudi nyumbani akiwa hai. Hatimaye baada ya shaka kumwondokea, alimkumbatia mwanawe. Mwangeka akajitupa kifuani mwa babake kwa furaha. Ridhaa alimkaribisha Mwangeka nyumbani na
kumtaarifu kuwa hakujua kuwa watawahi kukutana akiwa hai. Ridhaa akamjuwa mwanawe yaliyoisibu familia yao.


|