Mhusika Hazina na sifa zake katika riwaya ya chozi la heri
Answer Text: Mhusika Hazina na sifa zake-Kijana anayesaidiwa na Umu barabarani.a)Ni msomi.Alienda shuleni na kupata elimu. Uk 88,"Nilipelekwa shuleni nikasoma, nina elimu japo akali. Amesomea upishi na huduma za hotelini katika chuo.b) Mwenye upendo-Anamwita Umu anapomwona, kwa kukumbuka wema aliomtendea wakati mmoja. Hazina alimpeleka Umu kwenye hoteli na kumpa chakula mpaka akashiba. Aliahidi pia kumsaidia Umu, na akampeleka kwao nyumbani.(uk.89)