Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Yanayotokea katika sura ya nne ndani ya Chozi la heri

 (6m 49s)
10399 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya nne
-Mwangeka ameketi mkabala mwa kidimbwi cha kuogelea nje ya jumba lake la kifahari ambalo yeye aliliona kama makavazi ya kumtonesha donda
lililosababishwa na kifo cha mke wake Lily Nyamvula. Siku ile baada ya kutoka kwenye uwanja wa ndege walifululiza moja kwa moja hadi
kwenye gofu la baba yake Ridhaa. Majivu yaliyokuwa mabaki ya kilichokijwa kwenye kasri lile yalibaki pale pale. Majivu hayo miili ya mama yake(Terry), wanuna wake, mkewe na mtoto wake. Mwangeka hakuelewa ni kwa nini babake hakuyaondoa mabaki hayo na ni kwa nini hakushirikiana na majirani kuchimba kaburi (mass grave) kuyazika majivu hayo. Baba mtu alimkazia tu macho. Machozi mazito ya machozi yalitunga
machoni mwa Mwangeka, akayaacha yamcharaze yatakavyo.
-Wakati huu hata nyanya yake angekuwapo kumwonya dhidi ya kulia kama msichana angempuuza. Siku ile baada ya wao kutoka kwenye uwanja wa ndege, Ridhaa alimwelezea Mwangeka mambo yalivyojiri. Alimweleza kuwa maisha yalibadilika Pindi tu Mwangeka alipoondoka. Waliandamwa na msiba baada ya mwingine. Mwanzo, Ridhaa akapoteza majumba yake mawili. Miezi mitatu baadaye ami yake Mwangeka aliyeitwa Makaa alichomeka asibakie chochote alipokuwa aakiwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililokuwa limebingiria. Makaa alizikwa pamoja na mabaki ya wahasiriwa wote katika kaburi moja kwani serikali iliwatayarishia mazishi ya umma. Baada ya Ridhaa kushusha pumzi, aliendelea kum
- Weleza Mwangeka kuwa mambo hayo yote aliyakabili kwa msaada wa wanuna wa Mwangeka, mamake Mwangeka na rnkaza mwanawe. Akaanza
kuyajenga upya maisha yake hadi Siku ile ambayo aliitazama familia nzima ikimponyoka.


|