Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Yanayoshuhudiwa katika sura ya tano ndani ya chozi la heri

 (6m 31s)
7527 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya tano:
-Msitu wa Mamba uligeuka kuwa nyumbani kwa maelfu ya watu waliogura makwao bila tumaini la kurudi. Walijipa moyo na kusema kuwa hata
walikokuwa wakiishi hakukuwa kwao, walikuwa maskwota*. Wakaamua kula asali na kuyanywa maziwa ya Kanaani hii mpya isiyokuwa na
mwenyewe. Matokeo ya maamuzi haya yalikuwa ni kukatwa kwa miti kwa ajili ya kupata mashamba ya kupandia vyakula na kwa ajili ya ujenzi. Kabla ya miaka miwili kuisha, pahali hapa palikuwa pamepata
-sura mpya- majumba yenye mapaa ya vigae, misitu ya mahindi na maharage, maduka ya jumla, viduka vya rejareja kila mmoja akijibidiisha kufidia kile alikuwa amepoteza. Familia ya Bwana Kangata ilikuwa miongoni mwa zile zilizoselelea(zilizoishi) kwenye msitu huu. Kwa Kangata na mkewe
-Ndarine hapa palikuwa afadhali. Awali wakiwa wamelowea katika shamba Ia mwajiri wao aliyekuwa akiishi jijini. Waliishi pale kwa muda
mrefu hata watu wakadhani kuwa ilikuwa milki yao. Wengine wakidhani Kangata na familia yake walikuwa akraba ya mwajiri wao. Hata wana wa
Kangata walipokwenda shuleni walijisajilisha kwa jina Ia tajiri wa baba yao. Walikuwa wakiitwa Lunga
Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Kiriri likiwa jina Ia Mwajiri wa Kangata. Kazi aliyokuwa akiifanya katika afisi za umma kama mhazili mwandamizi kwa miaka mingi ilikuwa inamfanya kusinyaa, akawa hana hamau akahisi kinyaa. Wanawe walipoenda kusomea Ng'ambo - wafanyavyo wana wa viongozi kwa kuwa wanaiona elimu ya humu kama isiyowahakikishia mustakabali mwema raia wake, yeye alistaafu mapema na kuchukua kibunda cha mkupuo mmoja almaarufu
Golden Handshake akachukua Green Card na kuwafuata na kumwacha mume wake akiwa mpweke.


|