Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Yanayojiri katika sura ya tisa ndani ya chozi la heri

 (1m 57s)
8738 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya tisa:
-Sura hii inaanza kwa Wimbo wake Shamsi. Leo Ridha anamtazama Shamsi akipita kama afanyavyo kila siku. Shamsi anasikika kama amebadilisha wimbo wake kama anawosema Ridhaa japo kwa sauti ya chini. Wimbo huu wa leo unasikika kama wa kiumbe mwenye maumivu zaidi
na mapigo yake hasa ni ya mbolezi. Huu wa leo ni tofauti na majigambo yake ya kila siku.
-Ridhaa alianza kuyaghani majigambo yake Shamsi kwa sauti ya chini kama anayeyatia maneno ya majigambo kwenye mizani. Mtaa anakoishi Shamsi si mbali na hapa, Shamsi na Ridhaa ni majirani.
- Huu ni mwezi wa tatu tangu Ridhaa kuhamia mtaa wa Ahueni. Ahueni ni mtaa wa raia wenye kima cha juu kiuchurni. Mtaa huu una sura ya mijengo ya kifahari ya ghorofa. Daraja kubwa limeutenga mtaa huu na mtaa wa Kazikeni inakoishi familia ya Shamsi na nyingine za aina yake. Huko maisha ni ya kubahatisha. Huu ni mtaa wamabanda yaliyojengwa kwa udongo na mabati.
- Maisha ya Mwangeka sasa yalitengenea. Baada ya kuzungumza na mwanawe, Ridhaa alimwomba Mwangeka amruhusu aondoke ili akaanze kuyazoea maisha ya ujane. Aliondoka akiwa na azimio Ia kukamiIiSha kukijenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya alichokijenga kwenye ganjo lake. Kituo hicho kingewafaa raia wengi ambao hawangemudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi. Selume alifanya kazi katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya. Hali katika kituo hiki ni bora kuliko ilivyokuwa katika hospitali ya umma.
-Huko alikuwa amechoka kutokana na kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiiShia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali. Alikuwa amechoshwa na mambo mengi. Katika kituo hiki kipya Selume aliajiriwa kama Muuguzi Mkuu naye Kaizari. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Anaendelea kusema kuwa kupashwa tohara hakumaanishi kuacha Shule kwani dadake Hazina alipashwa tohara lakini sasa amehitimu shahada kutoka Chuo kikuu.
-Mgonjwa mwingine kwa jina Pete aliendelea kupata ahueni. Yeye aliokolewa akitaka kujiangamiza pamoja na kitoto chake. Pete alizaliwa katika kijiji cha Tokasa. Yeye ndiye mtoto wa nne katika familia yenye watoto sita.
-Pete kwa kuchelea kuiharibu ndoa yake akampagaza nyanya mzigo wa malezi. Pete hajadiriki kuonja tamu ya kupendwa na wazazi wake kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Alipojifungua, akaamua kwa mzee Fungo hakumweki tena.
-Kijakazi Sauna anatamani kurudi kitandani alale lakini inambidi amtayarishie Bi. Kangara kiamshakinywa kwani ana miadi ya mapema na mzalendo mmoja jijini. Anapojngia jikoni na kuanza shughuli zake moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili kusimama wima. Kwa mbali anaskia mbisho hafifu langoni mwa jumba hili.


|