Yanayojiri katika sura ya kumi katika chozi la heri
Answer Text: Sura ya kumi-Sura inapoanaza, Mwangemi anamrai Neema asiwe na mawazo finyu kuhusu kupanga mtoto. Anasisitiza kuwa hakuna udhaifu wowote katika kumpanga mtoto. Wamejaribu kupata mtoto kwa muda wa miaka mitano bila mafanikio. Neema amewahi kutunga mimba si mara moja aumbili, amefanikiwa kuilea mimba hadi ikakomaa wakaweza kukipakata kilaika mikononi mwao.- Kitoto hicho kiliaga kabla ya juma moja. Mwangemi na Neema walihuzunika kumpoteza mwana. Sio eti Neema hataki kumlea mwana, la hasha, anatamani kukipakata kilaika kiwe chake au cha mwingine. Mwangemi alimsihi Neema mke wake asijisulubu kwa kosa ambalo alilitenda kwa kutokuwa na ufahamu bora wa malimwengu. -Hayo yamepita. Baada ya Neema kukubali rai ya Mwangemi walienda katika kituo cha watoto cha Benefactor na leo hii wamo afisini. Walikaribishwana Mtawa Annastacia aliyewataarifu kuwa alilipata ombi Iao la kutaka kupanga mtoto kutoka kituo chao. Wakaelezwa kuwa kuna kijana mmoja wa kiume na iwapo wangefaulu katika mahojianO kituo hicho kingewakabidhi mtoto huyo.- Mahojiano yalipokamilika Mwangemi na Neema wakaondokawakitarajia kurudi kumchukua mwanao. Waliporudi afisini mwa Annastacia wana furaha mzomzo kwani walifaulu katika mahojiano nawako tayari kumchukua mwana wao. Mwangemi anahisi kuwa familia yake imekamilika. -Kijana huyu alipoletwa Mwangemi alimtulizia macho, kijana huyu ni mrefu na mwembamba, mwenye sura jamali. Macho yao yalipokutana kijana alitabasamu na kudhihirisha meno meupe pepepe ambayo yalimkumbusha binamu yake Mwangeka. -Hapohapo nyoyo zao zikaungana kila mmoja akijisemea kimyakimya, "Haikosi huyu atakuwa rafiki wa dhati " Mwaliko alitambulishwa kwa wazazi wake wapya. Kisha Mtawa Annastacia akamwahidi kuwa atakuwa akienda kumwangalia mara kwa mara.