Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Ufaafu wa anwani ya Chozi la Heri

 (10m 2s)
20560 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ufaafu wa anwani ya Chozi la Heri.
Kwa mujibu wa kamusi ya karne ya 21, CHOZI ni tone la maji au uowevu linalotoka machoni ambalo aghalabu hutokea mtu anapolia, kufurahi au moshi unapoingia machoni. Nalo jina HERI lina maana tatu:
1.Ni kuwepo kwa amani, utulivu na usalama
2.Ni hali ya kupata Baraka na mafanikio
3.Ni afadhali. Maneno haya yanapotumika pamoja tunapata maana iliyo na undani zaidi kuliko jina likitumika peke yake. Kwa hivyo, chozi la heri ni chozi ambalo linatoka wakati mhusika fulani amepata amani, utulivu na usalama. Chozi kwisha kupata baraka na mafanikio. Maana nyingine
ni kuwa chozi hili linaonekana ni chozi la afadhali. Kwa kujikita katika maana mbalimbali yanayojitokeza wakati maneno hayo mawili yamewekwa pamoja, matukio yafuatayo yanaafiki ufaafu wa CHOZI LA HERI.
i)Mwandishi anatuleza kuwa Ridhaa alipokwenda shuleni siku ya kwanza alitengwa na wenzake kwani hawakuta ashiriki michezo yao. Kijana mmoja
mchokozi alimwita 'mfuata mvua' aliyekuja kuwashinda katika mitihani yote. Ridhaa alifululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake. Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu keshoye.
ii)Ridhaa alipotoka kwenye Msitu wa Mamba alijiona nafuu kwani wapwa zake- Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu. Dadake Subira
alitibiwa akapona. Ridhaa anajua kuwa Kaizari ni afadhali kwa sababu hakuna aliyemtenga na mmoja kati ya jamaa zake. Ridhaa anapomfikiria Kaizari anajiambia heri nusu Shari kuliko Shari kamili.
iii)Ridhaa aliposikia sauti ya kike ikitangaza, tangazo lile lilimrudiSha katika mandhari yake ya sasa. Alijaribu kuangaza macho yake aone anakoenda
lakini macho yalijaa uzito wa machozi ambayo alikuwa ameyaacha yamchome na kutiririka yatakavyo.
iv)Wakati Ridhaa alimkazia macho Mwangeka-waka Mwangeka alikuwa akijiuliza iwapo babake amekuwa mwehu kwa kukosa kushirikiana na majirani kuchimba kaburi kuyazika majivu- matone mazito ya machozi yalitunga machoni mwake Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaza yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa macho haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo.
v)Wakati Ridhaa alikuwa akimsimulia Mwangeka.
vi)Katika Msitu wa Simba kulikuwa na maelfu watu waliogura makwao. Kati ya familia zilizoguria humu ni familia ya Bwana Kangata. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhali kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao. Uk 57.
vii)Wakati Neema na Mwangemi walikabidhiwa mtoto wao wa kupanga na Mtawa Annastacia, Mwaliko alimkumbatia Neema na kumwita mama na
kumwahidi kuwa ataenda naye. Neema alidondokwa na chozi la furaha na kumkumbatia Mwaliko kwa mapenzi ya mama mzazi. Hili lilikuwa ni chozila heri kwa familia hii yao


|