Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
OR
Processing. Please wait.
Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)
Maudhui katika riwaya ya Chozi la Heri
(16m 47s)
Download as pdf file
Answer Text:
Maudhui katika riwaya ya Chozi la Heri
i. Maudhui ya migogoro
Migogoro ni mivutano na mikinzano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Migogoro huweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka tofauti, nyadhifa mbalimbali, kiuchumi, nafasi katika jamii au hata kisiasa. Aina za migogoro katika riwaya hii.
a)Kuna mgogoro kwenye familia ya Mzee Mwimo Msubili, kwa sababu familia yake ilikuwa kubwa na hakuitosheleza kwa chakula. Uk 9,"Wingi wa vinywa vya kulishwa ulizua uhasama, migogoro na hata uhitaji mkubwa "
b)Mgogoro wa kijamii unajitokeza baada ya mkoloni kupuuza sera za Mwafrika. Uk 10.
c)Kulijitokeza mgogoro shuleni wakati Ridhaa aliitwa 'mfuata mvua',na kutengwa na wenzake. Walimwona kama mwizi. Uk 10,"Wewe ni mfuata mvua.
d) Ridhaa alijipata katika hali ya mgogoro na nafsi yake. Uk 12,"Miguu yake sasa ilianza kulalamika pole pole parafujo za mwili wake zililegea.
ii.Umaskini.
Umaskini ni ukata. Ni hali ya kukosa fedhamali nk. Tunapata kuwa waafrika wanajikuta katika hali ya umasikini; Uk 7,"Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogo wadogo, maskini, wasio na ardhi " Uk 25,"Nyinyi ndio vikaragosi wanaotumiwa na wasaliti wa nia zetu kuendelea kutudidimiza kwenye lindi hili la ukata " Ridhaa pia anajikuta kwenye lindi la umaskini baada ya mali yake yote kuchomwa, ikiwemo familia yake.
iii.Ushirikina.
Hii ni hali au tabia ya watu kuamini mambo ya utamaduni ambayo mara nyingi, yanajihusisha na uchawi. Ridhaa anaposikia milio ya bundi, anaamini kuwa milio hii ina maana iliyofichika. Uk 1,"Anakumbuka mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama. Milio hii ndiyo
iliyomtia kiwewe zaidi kwani bundi hawakuwa wageni wa kikaida katika janibu hizi "
iv.Ndoa.
Haya ni maafikiano rasmi baina ya mume na mke ili waweze kuishi pamoja. Kuna ndoa kati ya Ridhaa na Terry. akamgeukia mumewe tena na kusema, ...laiti Ridhaa angalijua kwamba hii ndiyo mara yake ya mwisho kuzungumza na mpenzi mkewe. Tunapata kuwa Ridhaa ana
mwoa Terry, uk ll "Baadaye aliamua kuasi ukapera, akapata mke, Terry " Mwangeka alikuta na Lily Nyamvula katika Chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto. Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa.
v.Mauti.
Hii ni hali ya kuiaga dunia wahusika wengine wanakutana na janga hili la mauti, ilhali wengine walio wakuu hawapatani nalo. Uk 2;Mamake Ridhaa aliiaga dunia na Ridhaa anakumbuka jinsi mamake alivyokuwa akimwambia "Moyo wa Ridhaa ulipiga kidoko ukataka kumwonya dhidi ya tabia hii ya kike ya kulia Pindi mtu akabiliwapo na vizingiti ambavyo ni kawaida ya maisha, ukamkumbusha maisha maneno ya marehemU mama yake siku za urijali wake " Terry na wana wake wanakumbana na janga la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao. Uk 3,"uuuui!uuuui!jamani
tuisaidieni!uuuui!uuuui!Mzee Kedi usituue!sisi tu majirani!maskini wanangu!maskini mume wangu!" Tunapata pia kuwa Kangata na mkewe Ndarine
wanakumbana na mauti. Uk 66; "Miaka mitano imepita. Kangata na mkewe Ndarine wameipa dunia kisogo "
vi.Ukoloni mambo leo.
Ukoloni mamboleo ni zao la uongozi mbaya. Viongozi waanzilishi wa mataifa yaliyopata uhuru hawakuzua sera na mikakati mwafaka ya kuhakikisha
nchi zao zimepata kujisimamia kiuchumi. Katika Chozi la Heri, Waafrika wenyewe wanajifanya wakoloni juu ya waafrika wenzao, ambao wako chini yao kitabaka au kisiasa kwa mfano katika ukurasa wa 5,mashamba ya Waafrika yananyakuliwa na watu binafsi baada ya wakoloni kwenda, nao waafrika wanawekwa mahali pamoja ili kuishi katika hali ya ujamaa "Lakini baba, wewe siwe uliyeniambia kuwa mashamba ya Theluji nyeusi yalikuwa milki ya wakoloni?na sasa yanamilikiwa na nani? N.k
vii.Ukoloni mkongwe.
Huu ni ukoloni uliokuwa wa Waingereza, kabla ya nchi za Afrika kupata uhuru. Tunapata kuwa mkoloni anapata fursa ya kuendeleza kilimo katika sehemu za mashamba ya Waafrika zilizotoa mazao mengi. Uk 7, "Mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya
mkoloni ilipompa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Katika ukurasa wa 7 tunasoma; "Waafrika
waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo, maskini, wasio na ardhi.
viii. Mapenzi.
Hii ni hali ya mvuto na upendo alionao mtu kwa mtu mwingine. Pia nia hisia ya upendo anayokuwa nayo mtu kuhusu mtu mwingine. Ridhaa alimpenda sana mkewe Terry na wana wake. "Polepole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya ma. jivu-la, juu ya miili ya wapenzi wake " Tunapata kuwa kuna mapenzi kati ya Mwangeka na baba yake Ridhaa. Haya ni mapenzi ya mzazi kwa mwanawe, Ridhaa alimpenda sana mwanawe Mwangeka kwani ndiye pekee tu aliweza kuepukana na janga Ia mauti kwa familia yote yake Ridhaa. Mapenzi haya yanadhihirika wakati Ridhaa anamlaki mwanawe kwenye uwanja wa ndege anapokuwa akirudi nyumbani kutoka ughaibuni.
ix.Ufeministi/ taasubi ya kiume.
Hii ni hali ambapo mwanamke anajidhalilisha ama anadhalilishwa katika jamii. Mwanamke hapewi nafasi katika jamii, ama anajiona kuwa kiumbe
dhaifu mwenye hana uwezo. Katika ukurasa wa 16 tunasoma; "Siku ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya, kiongozi ambaye kulingana na desturi za humu mwetu, hakustahili kuiongoza jamii ya wahafidhi na, kisa na maana, alikuwa mwanamke. Katika ukurasa wa 3;"Huku ni kujiumbua hasa. Unyonge haukuumbiwa majimbi; ulitunukiwa makoo.
|