Yanayotokea katika Sura ya saba ndani ya chozi la heri
Answer Text: Sura ya saba:-Ni alasiri moja ya joto kali. Mwangeka na Mkewe Apondi wameketi kwenye behewa la nyumba yao. Wameyaelekeza macho yao kwenye kidimbwiambamo wanao watatu-Sophie, Ridhaa na Umulkheri- wanaogelea. Ukichunguza kwa makini utapata kwamba wawili hawa chochote japo wanatazama. Kila mmoja, Apondi na Mwanageka, amepotea kwenye ulimwengu wake.-Mwangeka anapomtazama Apondi anatabasamu. Kisa cha kukutana kwao kilikuwa kama ifuatavyo: Miaka mitatu ya ujane ilikuwa imemdhihaki Mwangeka.Babake Mwangeka alikuwa akiishi nyumbani kwa Mwangeka kwa muda. Walikuwa wajane wawili waliokomaa. Hitaji la Mwangeka kuwa na mshirika wa kumwondolea ukiwa lilimwandama. Baba mtu alimtaka Mwangeka kuwazia suala hili, Alijua kuwa wakati ndio mwamuzi, ipo siku atakapotokeza hurulaini wake Mwangeka.- Ataifungua kufuli kubwa iliyoufunga moyo wake na hiyo itakuwa siku ya kumwaga chozi la heri. Baba mtu akaendelea kungojea kwa matarajio makuu, kila jioni akimchunguza mwanawe kuona kumetokea badiIikO lolote. Siku moja alikutana na RachaelApondi ambaye alifanya kazi katika Wizara ya Vijana na Masuala ya Kijinsia. Apondi alikuwa na shahada katika masuala ya kijamii. Apondi alikuwa mmoja wa wawasilishaji na ilipowadia zamu yake kuwasiliSha aliwasisilisha kwa ustadi wa hali ya juu. -Akauteka nyara moyo wa Mwangeka. Apondi alipotoka jukwaani alisindikizwa na makofi ya hadhira yake. Mwangeka akamsindikiza na macho zaidi ya makofi. Moyo wake uliokuwa umejaa barafu ukayeyuka na kutwaa uvuguvugu. Binti huyu alimkumbushaMwangeka marehemu mke wake Lily. Mwangeka na Apondi walipata kujuana vizuri zaidi wakati wa chamcha. -Huu ukawa mwanzo wa usuhuba na uchumba wa mwaka mwaka mmoja ambao kilele chake kilikuwa kufunga ndoa. Apondi alikuwa mjane wa marehemu Mandu. Mzee Mandu alijifiaughaibuni katika shughuli za kudumisha amani. Kifo chake Mandu kikamwachia Apondi na Sophie mwanawe wa miaka miwili kilio kisichomithilika.