Yanayojiri katika Sura ya kwanza ndani ya chozi la heri
Answer Text: Sura ya kwanza:-Sura hii inapoanza, Ridhaa alikuwa amesimama kwa maumivu makali huku mikono kairudisha nyuma ya mgongo wake uliopinda kwa uchungu. Amelitazama wingu la moshi ambalo linamkumbusha ukiwa aliozaliwa nao na ambao anahofia kuwa angeishi na kuzikwa nao.- Alipogeuka alitazamana ana kwa ana na moto ambao uliteketeza jumba lake la kifahari. Walioangamia mie ndani ni Terry (mkewe Ridhaa),bintiye Tila, Mkewe Mwangeka(Lily) na mjukuu wake Becky.- Tukio hill linamkumbusha mambo kadha yaliyotokea hapo awali yakiwemo mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama. Milio hii ilimtia kiwewe zaidi kwani bundi hawakuwa wageni wa kawaida katika janibuhizi. Alikumbuka akimwambia Terry kuwa milio hii ni kama mbiu ya mgambo ambayo ikilia huenda kukawa na jambo. -Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza ball alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini. Terry alishangaa ni vipi daktari mzima alikuja kujishughulisha na mambo ya ushirikina. Aliyakumbuka maneno ya marehemu mamake kuwa machozi ya mwanamme hayapaswi kuonekana mbele ya majabali ya maisha.- Siku hii Ridha hakujali la mama wala la baba; alijiskia kama mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululiziwa makonde bila mwombezi. -Anakumbuka mayowe ambapo mwenye kuyapiga alimsihi Mzee Kedi asiwauwe kwani wao ni majirani wake. Akamsihi asiwadhuru wanawe wala mume wake.- Baada ya mayowe haya ndipo alisikia mlipuko mkubwa kisha akashikwa na uziwi wa muda uliofuatwa na sauti nyingine ya Mkewe "Yamekwisha". Vita katika eneo hili ndivyo vilivyopelekea Ridhaa kupoteza familia yake na kubaki tu na Mwangeka.