Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Matukio ya sura ya pili katika riwaya ya Chozi la heri

 (10m 34s)
19520 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya pili
-Ni siku kumi tangu kuondoka kwa Kaizari na wenzake na kujipata katika mazingira haya mageni. Si mageni kwani ni mumo humo kwao kwani si ughaibuni wala nchi jirani.
-Pahali hapa ni kambi au mabanda yaliyosongamana. Waliokuwa nacho na wachochole wote wako pamoja katika kambi hii. Kuna kiasi fulani cha usawa. Japo wanasema kuwa wanadamu huwa sawa kifoni, kuna tofauti katika mandhari wanamofia. Kaizari anaanza kusimulia yaliyojiri siku ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.
-Anasema kuwa baada ya kutawazwa kwa kiongozi mwanamke(wengine waliamini hafai kuongoza) mambo yaliharibika. Watu wakashika silaha
kUPigania uhuru wao, uhuru ambao walidai
hawakupewa- Wakaupigania. Mwanaharakati mmoja kwa jina la Teitei akazidi kusema kuwa mwanamke kuiongoza jamii nzima
itakuwa kukivika kichwa cha kuku kilemba. Bi. Shali alikanusha kauli ya Teitei na kusema kuwa, Mwekevu(kiongozi mwanamke) alijitosa katika siasa
na kuomba kura kama wanaume hao wapinzani wake, akastahimili vitisho na matusi kutoka kwa wanaume na kwa hivyo ushindi wake ni zao Ia bidii
yake. Mradi wake wa kuchimba visima umewafaidi raia kwenye maeneo kame. Kaizari aliendelea kumweleza Ridhaa kuwa vita vilianza kati ya kundi lililokuwa linaunga mkono Mwekevu na lililokuwa likiunga mkono mpinzani
wake mwanamume.
-Vita vikacha- Cha baina ya pande zote mbili. Kundi pinzani likidai kuwa haiwezekani mwanamke kushinda uchaguzi huenda aliiba kura na wafuasi wake kuwanunua wanawake ambao ndio wapiga kura wengi. Kundi la mwekevu lilisikika likisema kuwa wakati wa mabadiliko ni sasa na kuwa wanastahili kumpa Mwekevu nafasi. MijadaIa iliyozuka ilizidisha migogoro na hali ya taharuki ikatamalaki. Askari wakatumiwa kudumisha usalama katika vijiji na mitaa. Muda si muda raia walianza kukimbizana na polisi. Katika mchezo huu, watu wengi walipoteza
maisha yao. Wengine walipoona kuwa mambo yameharibika waliacha makwao na kukimbia. Mali walioacha nyuma iliteketezwa. Sura ya nchi ya Wahafidhina ikawa mpya. Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina.
-Mizoga ya watu na wanyama, magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto na uharibifu wa mali na mazingira ukashamiri. Kaizari anakumbuka siku ya pili akiwa sebuleni na wanawe wakitazama runinga mara alisikia kuwa hakuna amani bila kuheshimu mwanamume.
Kilichofuatia ni mabarobaro waliobeba picha za mpinzani aliyeshindwa na Mwekevu na wakaanza kughani mkarara uliokuwa ukisema Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi wetu tawala Wahafidhina tawala. Juhudi za uongozi kurejesha hali kuwa ya kawaida ndizo zilizowafurusha wenyeji makwao.


|