Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
OR
Processing. Please wait.
Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)
Mbinu za lugha katika chozi la heri
(19m 55s)
Download as pdf file
Answer Text:
MBINU ZA LUGHA
(a) JAZANDA.
- Hii ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi. Katika ukurasa wa 4 tunasoma; "Mwangeka alisema Ridhaa kupitia kwa sauti ya mawazoni mwake, kumbe wewe ni
sawa na yule Mwangeka wa kihistoria ambaye kivuli chake kikitembea siku zote mbele yake, ambaye mwili wake ulikuwa kaka tu, roho yenyewe iliishi nje ya kaka hill kwa kutotaka kudhibi-tiwa? Umewezaje kunusurika?
(b) TASHIHISI/ UHUISHAJI.
- Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho uhai sifa za kiumbe mwenye uhai, au sifa za kibinadamu. Katika ukurasa wa 3 tunasoma; "Alijiona akiamka asubuhi ambayo ilizaa usiku wa jana, usiku ambao ulitandaza kiza katika maisha yake " Usiku unapewa sifa za kuwa na uhai na kupewa uwezo wa
kuzaa asubuhi kama mwana. Tunasoma; "Familia yangu na mali yote hii kuteketea siku moja?Bila shaka hili ni zao lingine la husuda"
- Katika ukurasa wa 35; "Undugu na utangamano wa wakimbizi wenzake uliyahuisha maisha yake, ukayajenga upya, ukamfunza Zaidi kuhusu
maisha yake, ukayajenga upya, ukamfunza Zaidi kuhusu thamani ya binadamu "
- Katika ukurasa wa 76; "Walipokuja hapa, ardhi hiyo haikuwa bikira, wakatifua udongo wakailima?"
- Katika ukurasa wa 143; "Kipanga sasa ameanza kuuhuisha utu wake "
(c) SEMI
- Semi ni fungu la maneno linalotumika kutoa maana tofauti na ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha.
- Kwa jumla, kuna aina mbili za semi.
a)Nahau
b)Misemo
- Katika ukurasa wa 2; "Wewe endelea kupiga hulu tu, lakini utakuja kuniambia "
- Katika ukurasa wa 3; "Angesema bibi huyu amebugia chumvi ya maisha ikamrishai
"Alijihisi kama mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululizwa makonde bila mwombezi "
- Katika ukurasa wa 6; "Na kazi zenyewe si kazi, ni vibarua vya kijungujiko tu'
(d) METHALI
- Hii ni misemo ya hekima yenye maana
iliyofumbwa. Mwandishi hutumia methali kupitisha ujumbe fulani. Katika ukurasa wa 12; "Kweli jaza ya hisani ni madhila?"
- Katika ukurasa wa 51; "Alimtazama baba yake kana kwamba anataka kuhakikishiwa jambo, naye Ridhaa akamjibu kwa mtazamo uliojaa Imani,
"Mwenye macho haambiwi tazama"
- Katika ukurasa wa 53; "Akili yake ilimkumbusha methali aliyozoea kumtolea mpinzani wake darasani kila mara Mwangeka alipomshinda kuwa, 'Wino wa mungu haufutikiā€¯
(e) LAKABU.
- Ni mbinu ya mhusika kupewa ama kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia au sifa zake.
- Katika ukurasa wa 94, "Haikuwa ibra kumsikia nyanya akimrejelea mama
kama Muki, yaani, huyo wa kuja, na kusema kwamba msichana wa bamwezi, hata akiwa na umri wa miaka tisini, ni msichana wa Bamwezi tu.
- Katika ukurasa wa 178; "Pongezi engineer Vuuk. Naona hili litatusaidia kumhepa Kumuku mwenye kuchungulia
kutoka dirisha ndogo la kibanda chake.
(f) RITIFAA
- Hii ni mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa au asiyekuwepo kana kwambo yupo pamoja nawe.
- Katika ukurasa wa 6; "Ni kweli binti yangu, kwa kutumia falsafa hii, una
haki ya kusema Sisi tu watoto wa miaka hamsini;
- Katika ukurasa wa 12; "Ridhaa hakujua majibu ya maswali haya. Alilojua ni kwamba haya siyo aliyotumaini baada ya miongo mitano ya maisha katika maskani haya. Alitamani kupiga ukemi kumwamsha mkewe lakini akili ilimkumbusha kuwa
huyo hayupo tena katika ulimwengu huu.
(g) TAASHIRA.
- Haya ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.
- Katika ukurasa wa 3; "Katikati ya mito hii ya machozi, Ridhaa aliileta picha ya maisha yake mbele ya kipaji chake"
- Katika ukurasa wa 5; "Lakini baba, wewe siwe uliyeniambia kuwa mashamba ya theluji nyeusi yalikuwa milki ya wakoloni?
- Katika ukurasa wa 12; "Ridhaa hakujua alikuwa amesimama pale kwa muda gani. Miguu yake sasa ilianza kulalamika. Pole pole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya majivu-la juu ya miili ya wapenzi wake".
(h) TAKRIRI.
- Hii ni mbinu ya kurudia rudia neno moja au fungu la maneno ili kusisitiza ujumbe Fulani.
- Katika ukurasa wa 4; "Ridhaa alirudi nyumbani na kusimama katikati mwa chumba ambacho yeye na aila yake walikuwa wamekitumia kama sebule kwa miaka na mikaka "
- Katika ukurasa wa 14; "Na usidhani ni mazingira mageni, kweli si mageni, si mageni kwani tu mumu humu mwetu, hatumo ughaibuni wala nchi jirani.
(i) TASWIRA
- Haya ni matumizi ya maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji. Ni mchoro au picha ya kitu
au hali fulani inayotokea katika fikira za mtu asomapo kazi ya kifasihi
- Katika ukurasa wa 7; Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo.
- Katika ukurasa wa 15;Jua lilichomoza, halina ule wekundu wa jua Ia matlai ambao huleta haiba ya uzawa wa siku yenye matumaini.
- Katika ukurasa wa 47; "Nakusikitikia mwanangu, kuwa huna hata familia ya kuendea. Wanuna wako wote wameangamia.
|