Uchambuzi wa sura ya nane katika Chozi la heri
Answer Text: Sura ya nane-Siku hii Dick alihisi kuwa uwanja wa ndege ulikuwa na baridi na mzizimo kuliko siku nyingine zote. Dick alikuwa akiwaza haya akiwa kasimama katika mlolongo mkubwa wa watu ambao walingoja kuingia kwenye afisi za forodha kukaguliwa. Akawa anakumbuka siku alipoanza kusafiri kwandege. Siku hiyo alijawa na kiwewe kwani biashara haramu ya kubeba dawa za kulevya aliyokuwa amejiingiza kwayo ilikuwa irnewaingiza wengikwenye mikono ya polisi, wakatiwa mbaroni. -Siku hizo alikuwa mwanagenzi katika uga huu kwani alikuwa na umri wa miaka kumi tu. Zipo sikualipotetemeka karibu ajisaliti lakini hatimaye alizoea kujipa moyo. Sasa miaka kumi ya adha imepita. Alilazimika kukomaa kwa kuwa ulimwenguhaukuhitaji mnyonge. Dick alitoswa katika kinamasi cha kuuza dawa za kulevya na Sauna- kijakazi wao. Dick amesafirisha maelfu kwa maelfu ya vifurushi vya dawa hizi. Mwanzoni akawa si mraibu wa dawa hizi lakini ilibidi ajizoeshe kwa usalama wake mwenyewe, kwani mara nyingi alilazimika kuzimeza dawa zenyewe ili kwenda kuzitapika kwenye masoko ya ughaibuni. -Jambo hili lilichangiwa na uwepo wa mashine zenye uwezo mkubwa wa kung'amua shehena za dawa zilizofichwa kwenye chupi. Siku ile baada ya kijakazi Sauna kumwiba Dick Alimpelekea baba mmoja tajiri ambaye alijitia kumpeleka shuleni. Kumbe alikuwa amempeleka katika biashara ya kuuza dawa za kulevya. Buda ( lakabu ya tajiri wake Dick) alipoona Dick akitaka kukataa kushiriki biasharahii, alimtishia Dick kuwa angetupwa nje, asingiziwe wizi na bila shaka Dick alijua malipo ya wezi ni kutiwatairi na kuchomwa moto. Wazo la kupata adhabu ya aina hii lilimtetemesha Dick. Akambuka rafiki yake Lemi alivyofishwa kwa njia hii. Kisa cha Lemikilimfanya kuunasihi moyo wake kuingilia biashara hii haramu ili mwenye nguvu asije akamtumbukiza kaburini. Wakati Dick alikuwa akiwaza kuhusu familia yake, hakujua kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake kapiga foleni. -Anasafiri ng'ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake. Kisadfa, safari ya Umu imekuwa siku hii ambapo Dick anasafiri. Dick aliposikia Mwangeka akimwita Umu na kumtaarifu kuwa ndege i karibu kuondoka, hakuamini.- Mazungumzo baina ya Umu na wazazi wake yalimwamsha Dick kutoka lepe lake la muda. Aligeuka na kutazamana ana kwa ana na Umu. Mwanzoni Umu akidhani macho yanamdanganya. Mikono yake ikamwachilia dadake Sophie, moyo wake ukamwenda mbio. Ghafla Dick, alimwita dadake Umu nakumkimbilia. Wakakumbatiana. Wasafiri wote na aila yote ikawatazama kwa mshangao. Machozi yakawadondoka wote wawili na kulia kimyakimyahuku wakiambiana kimoyomoyo yote yaliyowakumba. Hatimaye sauti iliita ikitangaza kuwa abiria wa ndege Tumaini waanze kuingia.