Mhusika Mzee Kaizari na sifa zake katika riwaya ya Chozi la heri
Answer Text: Mhusika Mzee Kaizari.Alikuwa babake Mwanaheri, na Lime.Sifa.a)Mwenye Busara.-Aliyajenga maisha ya familia yake upya baada ya kutoka msituni na kurudi nyumbani.(uk 93)b)Mwenye mapenzi kwa familia yake.Aliweza kuijengea familia yake nyumba pale ambapo waliishi zamani. Baada ya mkewe kutoweka, tunamwona Mzee Kaizari akitia bidii sana katikakumtafuta kwao na pia mjini.(uk.96)c)Mvumilivu.Anapompata mkewe akiwa ameaga dunia, alivumilia uchungu wa kumpoteza ampendaye, na akamzoazoa na kumzika pamoja na wanawe.(u.k.96)