Jalada la Chozi la Heri
Answer Text: Jalada la Chozi la Heri-Assumpta.K.Matei-Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri ni tokeo la usanii wake , Robert Kambo. Katika upande wa mbele sehemu ya juu, mna rangi ya kijani kibichi iliyokolea. Maana ya rangi hii ni uhai na rutuba. Riwayani yamo maeneo yaliyo na rutuba yanayotoa mazao mengi. Katika eneo la Msitu wa Heri alikoishi Ridhaa kwa miongo mitano, mwanzoni kulikuwa kama jangwa la Kalahari lakini Ridhaa alihakikisha kuwa kijiji hikikimepata maji ya mabomba hadi eneo zima likatwaa rangi ya chanikiwiti.- Kwenye msitu wa Mamba,watu waliogura makwao walipohamia hapa walikata miti na kupanda vyakula kama mahindi ambayo yalifanya vizuri mno. Ndani ya rangi hii mna anwani ya kazi iliyoandikwakwa rangi nyeupe. Kawaida rangi hii huashiria amani. -Licha ya mambo kuwaendea vibaya wahusika wengi riwayani, hatimaye mna amani ya kudumu. Jina lake mwandishi liko maeneo yayo hayo na limeandikwa kwa rangi ya manjano. Rangi hii huashira ukomavu. Mwandishi wa riwaya hii nimwenye tajriba pana. Amekomaa katika uandishi wa kazi za fasihi.- Upande wa chini wa jalada la riwaya hii mna mchoro wa jicho. Jicho hili linadondokwa na chozi. Ndani ya chozi mna watu watatu(mmoja wa kike na wawili wa kiume). Inahalisi kuwa watu hawa watatu ni Umu,Dick na Mwaliko. Walifurahl mno walipokutana wote katika hoteli ya Majaliwa.- Riwayani, Umu na Dick walikimbia wote kwa pamoja na wakamkumbatia ndugu yao Mwaliko na huku wakaanza kulia na kutokwa na machozi ya farajaheri.