Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Riwaya ya Chozi La Heri (Assumpta K. Matei)

Yanayotokea katika sura ya sita katika chozi la heri

 (8m 7s)
9376 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sura ya sita:
-Sura hii inapoanza tunampata Mwalimu Dhahabu akimtaka Umulkheri kuyarudisha mawazo yake darasani. mwalimu huyu kwa kawaida ni mcheshi. Umu(ufupi wa Umulkheri) aliyarudisha macho yake darasani yakatazamana na ya Mwalimu Dhahabu bila yeye Umu kumwona mwalimu mwenyewe. --Tangu Umu kujiunga na Shule hii katika kidato cha pili anajihisi kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Haya mazingira ni mageni kwake na hakuja hapa kwa hiari. Baridi ya mahali hapa inamsinya kwani si kama kwao ambako kulikuwa na hari*. Ukweli ni kuwa Umu alikuwa na kwao ila sasa hana. Amebaki kuishi kwa hisani ya mkuu wa Shule ya gamano aliyeshauriwa na Wizara ya Elimu kumsajili umu na wengine watano. Umu ni mwana wa pili wa Bwana Lunga
Kiriri —Kangata. Uongozi ulipoamua kuwahamisha hadi mlima wa Simba, IJmu alikuwa ndio anajiunga na kidato cha kwanza. Kule kuhamia Mlima wa Simba hakukumkalia vyema Lunga. Aliona kuwa alikuwa ameyapoteza maisha yake pamoja na ndugu na marafiki zake. Wanawe walikuwa wakisomea katika Shule za kifahari na sasa fidia aliyopewa na serikali haitoshi hata kuwapeleka wanawe katika Shule za watu wa kima wastani.
-Akawaacha Lunga na wanawe. Pigo hili la tatu lilimuuma Lunga sana kwani alijisabilia kwa hali na mali kumpendeza mkewe.
Naomi alilipa penzi lake na kumwachia Lunga adha za malezi jambo ambalo Lunga hakustahimili. Mwaka
mmoja wa kwanza ulimwia Lunga mgumu mno kwani ilimlazimu Lunga kuwa mama na baba wa watoto wake. Asubuhi moja IJmu aliamka na kujipata yu pweke nyumbani mwao. Ndugu zake wawili, Dick na Mwaliko walikuwa wametoweka. IJmu alijaribu kumwita kijakazi Sauna kumjuza lakini alisalimiwa na cheko la mwangwi wa sauti yake katika sebule. umu alimaka, hajui awafuate wapi ndugu zake
wakembe.
-Dick alikuwa darasa la saba naye mwaliko alikuwa katika darasa Ia kwanza. Picha ya watoto waliotekwa nyara ilimjia Umu akilini mwake ikakifanya kichwa chake kumwanga kwa maumivu.


|