Sifa za mhusika Ridhaa katika riwaya ya chozi la heri
Answer Text: Sifa za mhusika RidhaaHuyu ni mumewe Terry. Ni mhusika mkuu ambaye ana sifa kadhaa.Sifa(a) Mshirikina.Uk 1,"Anakumbuka mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama. Milio hiyo ndiyo iliyomtia kiwewe zaidi kwani bundi hawakuwa wageni wa kikaida katika janibu hizi "(b) Mwepesi wa moyo.Ridhaa ni mwepesi wa moyo kwani anapopatwa na mawazo ya hapo awali ambayo ni ya kukatisha tamaa, analia kwa urahisi, kinyume na matarajio ya jamii kuwa mwanaume hafai kulia.(uk 105).(c) Mwenye bidii. Uk 4,"Alikuwa amesafirikwa shughuli za ujenzi wa taifa, ka-ma alivyoziita safari zake za kikazi " Tunapata kuwa Ridhaa alikuwa ni mwenye bidii za mchwa katika kazi yake ya kila siku aliyoiita 'ujenzi wa taifa'.(d) Mvumilivu.Aliweza kuvumilia matukio yaliyomkumba kijijini mwake, yakiwemo kutotakwa huko, na kufukuzwa, mali yake kuharibiwa na familia yake kuuliwa. Anapiga moyo konde kukabiliana na hall hiyo mpya (uk 25).