``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’a)Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili. (alama 10)d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. ( alama 4)
Answer Text: ``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’a)Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)i) hii ni kauli ya mwandishiii) anarejelea tukio la ulafi wa Jituiii) mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Magoiv) watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitub) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)i) nahau- kukiangua kitendawiliii) jazanda - neno kitendawili kurejelea jambo fulani lililofichikac) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawilikinachorejelewa katika dondoo hili. (alama 10)i)Kuwepo kwa uvumi na nong`ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya Wanamadongoporomoka.ii)Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.iii)Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki za Wanamadongoporomoko inayofanyika katika mkahawa.iv)Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharukiHatima- Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.i)Hatimaye jitu kufika na mabuldozaii)Askari wa baraza kuandamana na jituiii)Jeshi la polisi kuwalinda askari wa barazaiv)Watu kupigwa virungu bila hatiav)Vibanda kubomolewad) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. ( alama 4)i)Wazalendo halisi; wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumiliki na kukomboa ardhi yao.ii)Wenye bidii: hawasiti /hawakomi kuandaa mikakatiya kupigania haki zao . mfano: mikutano yao.iii)Wenye umoja na ushirikiano : wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi wa haki zao.iv) Wakakamavu/ jasiri: wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao iliyonyakuliwa.v)Wenye hekima/ busara: wanabaini hila za wenye nguvu kutaka kunyakua ardhi yao na kujiandaa kukabiliana nao.