Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a). Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
b). Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili (Alama 2)
c). Fafanua kile kilichokuwa kikitokea (Alama 2)
d). Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke (Alama 12)

 (6m 34s)
2972 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
Mnenaji – msimulizi
Mnenewa – anawarejelea wenyeji wa Madongoporomoka
Mahali – vibandani katika eneo la Madongoporomoka
Sababu – Mabuldoza yalikuwa yameanza kubomoa vibanda vya watu wa Madongoporomoka.
b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili (Alama 2)
Tashihisi Akili zao zilipowaamsha kuwapaleka kwenye maana hasa
c. Fafanua kile kilichokuwa kikitokea (Alama 2)
Vibanda vya watu wa Madongoporomoka vilikuwa vikibomolewa bila huruma.
Jeshi la polisi lililokuwa limeshika bunduki lilisimamia mabuldoza yakibomoa vibanda
Watu waliokuwa wamelala walitimuliwa
Askari wa baraza la jiji walikuwa wanabomoa vibanda
Kulikuwa na muangaiko hasa kwa watu wa Madongoporomoka
d. Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke (Alama 12)
-Watu walikuwa wanafanya kikao katika hoteli yam mzee Mago kujadili namna ya kuzuia kubomolewa vibanda vyao
-Kutafuta wanasheria waaminifu ili kutatua sitofahamu
-Mzee Mago alishinda kuwazindua
Wanadongoporomoka kuchunguza maendeleo yanayozungumziwa kama yangeleta manufaa au hasara
-Mzee Mago aliwaleta watu Madongoporomoka pamoja ili kutetea haki ya kumiliki ardhi ya Madongoporomoka
-Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawangeweza, kwani wanaogopa umma wa Madongoporomoka
-Wanyonge walishikilia kauli yao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katika ardhi yao
-Baada ya majuma matatu ya vurugu vibanda mshenzi vya Madongoporomoka viliota tena vingi kuliko vya awali.


|