Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Jadili mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”

 (8m 4s)
14861 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka” (alama 20)
Mhusika ni Mashaka aliyepata mikasa mingi maishani mwake tangu alipozaliwa. Kwanza mama yake Ma Mtumwa alifariki alipomkopoa tu, kutokana na kifafa cha uzazi.Babake yake naye upweke ulimshinda akafariki na wakazikwa pamoja. Mashaka hakuwahi kuwaona hata kwa sura, hivyo
hawakumbuki. Biti Kidebe ndiye aliyemlea kwa shida na makuzi yalikuwa ya taabu – makuzi ya tikitimaji au tango kuponea umande.Biti Kidebe alikuwa haishi kulalamikia miguu yake iliyomuuma. Hivyo, licha ya yeye kumlea Mashaka, naye Mashaka akamlea huyu bibi. Alitafuta kila aina ya vijikazi alivyoviweza tangu akiwa mtoto. Biti Kidebe aliwahi kumsomesha kwa shida hadi
darasa la nane. Mashka anapata mke akiwa hana chochote kwa kuozwa kwake Waridi. Ndoa hii ilimtia Rubeya aibu kwa kuwa binti yake ameolewa na fukara. Mzee Rubeya na familia yake wakaamua kurudi kwao Yemeni. Mashaka na Waridi waliishi katika mtaa wa watu wa hali ya chini (fukara) uitwao Tandale. Mandhari ya chumba chao kimoja yalikuwa kando ya choo
kilichofurika vibaya wakati wa mvua na kueneza kinyesi kila mahali. Kulikuwa na uvundo uliotisha kwenye nyumba yao daima. Chumba chao kilivuja wakati wa mvua. Wakati huu wanapata tabu sana. Mashaka na Waridi walipata watoto saba. Hivyo ilikuwa shida watu tisa kuishi kwenye chumba kimoja. Mashaka alikuwa na kazi duni yenye mshahara wa mkia wa mbuzi – alikuwa mlinzi wa
usiku katika kampuni za Zuia Wizi Security (ZWS). Watoto wake wavulana walilala jikoni kwa jirani Chakupewa.


|