“ Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.”
Answer Text: “ Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.”-Tumbo kubwa linalokula bila kujaa ni Jazanda ya vitendo vya matajiri wenye tama ajabu ya kunyakua bila kukoma mali ya maskini-Jitu la miraba minne ni jazanda ya matajiri wakubwa ambao wanatumia nafasi yao kuwakandamiza maskini.-Jitu linaingia kimiujiza bila kujulikana. Kuingia kwa ghafla ni Jazanda ya jinsi matajiri hawa wanavyovamia na kunyakua mali ya maskini bila kutarajiwa.-Jitu kukalia meza inayoweza kutoshea watu wane ni Jazanda ya matajiri kuvamia na kunyakua ardhi/mali ya maskini wengi.-Kiti kulalamika na meza kuonekana ndogo ni jazanda ya dhuluma na ukatili wamatajiri hawa kwa wananchi wenye uwezo mdogo.-Jimwili na tumbo kubwa lililolalia meza ni jazanda ya utajiri na uwezo wao wa kifedha. Tumbo kubwa pia ni jazanda ya uroho/ulafi wa mali/hawatosheki.-Jitu kubwa kufagia chakula chote hotelini na kuwamalizia wengine ni jazanda ya jinsi amabavyo matajiri wanaparamia mali/ardhi yawananchi maskini bila kuwabakishia chochote .-Jitu kuja kula katika hoteli uchwara ya mzee Mago ni jazanda ya jinsi matajiri yangekuja kuinyakua ardhi ya maskini.-Kitendo cha jitu kula na kuramba sahani ni jazanda ya ulafi wa matajiri tapeli ambao tamaa yao haiwezi ikamithilishwa na chochote.